SHANGWE ZA 'SELEBRETIKA KIJAMUKAYA' MSIMU WA SIKUKUU ZATUA KWA WAZAZI KITUO CHA AFYA KAMBARAGE

Mmoja wa akina mama katika Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga akiishukuru Kampuni ya Jambo Group kwa kuwapatia bidhaa maalum za Jambo Group kwa ajili ya Msimu wa Sikukuu
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa wa Kampuni ya Jambo Group, Nickson George (wa pili kushoto) akikabidhi bidhaa maalum za Jambo Group Msimu wa Sikukuu kwa ajili ya akina mama wajawazito na waliojifungua katika Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
 Kiongozi Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa wa Kampuni ya Jambo Group, Nickson George akikabidhi bidhaa  maalum za Jambo Group  msimu wa sikukuu kwa mmoja wa akina mama katika Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa wa Kampuni ya Jambo Group, Nickson George (wa pili kushoto) akizungumza wakati akikabidhi bidhaa maalum za Jambo Group Msimu wa Sikukuu kwa ajili ya akina mama wajawazito na waliojifungua katika Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kampeni ya Selebretika Kijamukaya 'Sisi Ndio Sikukuu Yenyewe' inayoendeshwa na Kampuni ya Jambo Group Msimu huu wa Sikukuu imezinduliwa rasmi na sasa imefika katika Kituo cha Afya Kambarage kilichopo Manispaa ya Shinyanga. 

Katika hatua hiyo, akina mama wajawazito na waliojifungua wamefikiwa na kufurahia bidhaa maalumu za Jambo, ikiwa ni pamoja na biskuti na vinywaji vyenye chapa au logo maalum ya Jambo Msimu wa Sikukuu, vyote vikiwa na ladha ya sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya 2025.

Kampeni hii ilizinduliwa rasmi Desemba 21, 2024, kwenye Ofisi za Jambo Media zilizopo Ibadakuli Mjini Shinyanga.

Kiongozi Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa wa Kampuni ya Jambo Group, Nickson George, amesema kampeni hiyo ni sehemu ya juhudi za kuwafikia wateja na watumiaji wa bidhaa za kampuni hiyo, ili waweze kufurahia bidhaa za Jambo na familia zao wakati wa msimu wa sikukuu.

“Lengo letu ni kuleta furaha na ladha ya Jamukaya kwa familia nyumbani, hivyo tumekuja na vinywaji maalumu vyenye logo ya Jambo ili kufanya sikukuu iwe tamu zaidi. Vinywaji vyetu pia ni vya manufaa kwa afya, kwa sababu vina sukari rafiki kwa wale wanaochangia damu,” amesema George.

Kiongozi Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa wa Kampuni ya Jambo Group, Nickson George (kushoto) akizungumza wakati akikabidhi bidhaa maalum za Jambo Group Msimu wa Sikukuu katika Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga

Ameeleza kuwa baadhi ya vinywaji vya kampuni hiyo vitahifadhiwa kwenye benki ya damu ya Kituo hicho cha afya, na kwamba wananchi watakaohudhuria kutoa damu watapewa vinywaji hivyo kama sehemu ya mchango wao katika kuokoa uhai. 

Amesisitiza kuwa vinywaji vya Jambo, ambavyo vimebeba ladha ya Sikukuu, vitakuwa na manufaa kwa watu wote, hasa wale watakaoshiriki katika michango ya damu, kwani vina sukari rafiki kwa afya na vinasaidia kuongeza nguvu.

Amefafanua kuwa, Kampeni ya Selebretika Kijamukaya inalenga kuhamasisha jamii kufurahia bidhaa za Jambo na kusaidia kuokoa maisha kwa kuchangia damu wakati wa msimu wa sikukuu.

“Mwenyekiti wa Kampuni za Jambo Salum Khamis hakuanzisha kampuni hizi kwa ajili ya kupata faida tu,bali ni kugusa pia maisha ya watu,na ndiyo maana leo tumeamua kuleta furaha kwa wagonjwa na watumishi wa kituo hiki cha Afya Kambarage kwa kuwapatia vinywaji na biskuti zenye chapa ya Selebretika Kijamukaya kwa ajili ya kufurahia msimu wa sikukuu,”ameongeza George.

Ameongeza kuwa ili familia iweze kufurahia sikukuu ipasavyo, bidhaa za Jambo zinapaswa kuwa sehemu ya meza ya chakula kila siku: Asubuhi ukiamka, vitafunwa vya Jambo, maji ya Jambo, juisi za Jambo, biskuti za Jambo, Ice Cream za Jambo - bidhaa hizi zitafanya sikukuu iwe yenye ladha ya kipekee.

 Kampeni ya Selebretika Kijamukaya inaendelea kuhamasisha watu kufurahia bidhaa za Jambo wakati wa msimu wa sikukuu na kuhakikisha kuwa nyumbani kunakuwa na ladha ya Jambo muda wote.

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kambarage, Ernest Magula, pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Kituo hicho, Adolf Nsanzungwanko, wameishukuru Kampuni ya Jambo Group kwa kutoa zawadi za Sikukuu kwa wagonjwa, wakiwemo akina mama wajawazito na waliojifungua katika msimu huu wa Krismasi na Mwaka Mpya.

Magula na Nsanzungwanko wameeleza kuwa zawadi hizo zimeleta faraja kwa wagonjwa, huku wakisisitiza umuhimu wa ushirikiano na wadau wengine ili kuendelea kusaidia katika kuboresha huduma za afya. 

Wamesema changamoto zinazokikabili kituo hicho ni pamoja na upungufu wa damu salama na ukosefu wa uzio wa kuimarisha usalama.

Kwa upande wao, akina mama waliokutwa katika wodi ya wazazi, akiwemo Fortunatha Athanas na Juliana Shija, wameishukuru Kampuni ya Jambo Group kwa kutoa zawadi hizo za Sikukuu, huku wakiipongeza kwa ubunifu wake. 

Wamesisitiza kuwa watendelea kutumia bidhaa za Jambo hata majumbani mwao kwa sababu wanaziamini na kuzithamini.

Kiongozi Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa wa Kampuni ya Jambo Group, Nickson George (katikati) akizungumza katika Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga leo Desemba 22,2024 wakati akikabidhi bidhaa maalum za Jambo Group Msimu wa Sikukuu kwa ajili ya akina mama wajawazito na waliojifungua katika kituo hicho cha afya - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa wa Kampuni ya Jambo Group, Nickson George (wa pili kushoto) akikabidhi bidhaa maalum za Jambo Group Msimu wa Sikukuu kwa ajili ya akina mama wajawazito na waliojifungua katika Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Sehemu ya bidhaa za Jambo Group zenye chapa/logo ya Jambo zilizokabidhiwa na Jambo Group kwa akina mama wajawazito na waliojifungua katika Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa wa Kampuni ya Jambo Group, Nickson George akikabidhi bidhaa  maalum za Jambo Group  msimu wa sikukuu kwa mmoja wa akina mama katika Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa wa Kampuni ya Jambo Group, Nickson George akikabidhi bidhaa  maalum za Jambo Group  msimu wa sikukuu kwa mmoja wa akina mama katika Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa wa Kampuni ya Jambo Group, Nickson George akikabidhi bidhaa  maalum za Jambo Group  msimu wa sikukuu kwa mmoja wa akina mama katika Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa wa Kampuni ya Jambo Group, Nickson George akikabidhi bidhaa  maalum za Jambo Group  msimu wa sikukuu kwa mmoja wa akina mama katika Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa wa Kampuni ya Jambo Group, Nickson George akikabidhi bidhaa  maalum za Jambo Group  msimu wa sikukuu kwa mmoja wa akina mama katika Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa wa Kampuni ya Jambo Group, Nickson George akikabidhi bidhaa  maalum za Jambo Group  msimu wa sikukuu kwa mmoja wa akina mama katika Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Kiongozi Mkuu wa Jambo Media na Kiongozi wa Ubunifu na Chapa wa Kampuni ya Jambo Group, Nickson George (kushoto) akizungumza wakati akikabidhi bidhaa maalum za Jambo Group msimu wa sikukuu kwa akina mama wajawazito na waliojifungua katika Kituo cha Afya Kambarage Manispaa ya Shinyanga

Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Kambarage, Ernest Magula akizungumza wakati Jambo Group ikikabidhi bidhaa maalum za Jambo Group msimu wa sikukuu kwa akina mama wajawazito na waliojifungua katika Kituo cha Afya Kambarage

Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Kituo cha Afya Kambarage, Adolf Nsanzungwanko akizungumza wakati Jambo Group ikikabidhi bidhaa maalum za Jambo Group msimu wa sikukuu kwa akina mama wajawazito na waliojifungua katika Kituo cha Afya Kambarage.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA