TGNP KATIKA UTEKELEZAJI MRADI WA "TUINUKE PAMOJA" KUWANUFAISHA MAKUNDI YA VIJANA, WANAWAKE NA WATU WENYE ULEMAVU



Na, Mwandishi wetu - Dodoma.

Kikao cha wadau wa mradi wa 'Tuinuke Pamoja' kimewakutanisha wawakilishi kutoka Wizara mama ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi maalum, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Halmashauri za Wilaya ya Chemaba na Kondoa, wawakilishi wa AZAKI, watendaji wa Agha Khan Foundation (AKF) na watendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).


Kikao hicho kilichofanyika leo tarehe 06/12/2024 Jijini Dodoma Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania Lilian Liundi  amesema kikao hicho ni mahususi kwa ajili ya kupitia muongozo ambao ulishatolewa hapo awali wa kutambua vikundi vya kijamii vitakavyoshiriki katika mradi huo ili kufanya maboresho.


Amebainisha kuwa mwongozo wa kutambua vikundi vya kijamii vitakavyoshiriki katika mradi wa Tuinuke pamoja kwani wana lenga kupata maboresho na thibitisho la mwongozo utakaotumika kutambua vikundi hivyo vya kijamii vitakavyojengewa uwezo na kuwezeshwa kifedha kuendeleza harakati zao katika kuleta usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake katika jami zao.


“Moja ya afua muhimu sana inayoweka msingi wa utekelezaji wa mradi huu ni utambuzi wa Asasi za Kiraia, Mashirika yanayotetea haki za wanawake, Vikundi vya kijamii, vikiwemo vituo vya Taarifa na Maarifa, majukwaa na mitandao mbalimbali iliyopo kitaifa, kiwilaya na katika ngazi ya chini kabisa ya jamii,” alisema Liundi.


Aidha ameongeza kuwa utambuzi huo unawezesha utelekezaji wa mradi hasa katika lengo lake mahususi la 3 lenye kulenga kuunganisha vikundi na wadau, majukwaa na mitandao mbalimbali inayofanya kazi kama watakazokuwa wakifanya wao ili kuimarisha harakati zao na kuwasaidia kuunganisha nguvu na sauti katika kufanya chechemuzi.


Kwa upande wake Afisa maendeleo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Elizabeth Shoo ameshukuru ushirikiano wa mashirika ya TGNP na AKF kwa namna ambavyo walianzia chini kwa ngazi ya jamii kwa kuvitafuta, kuvisikiliza na kufanya utafiti lengo likiwa ni kuleta tija ya mradi.


Amesema kwa mchakato huo ni imani yao mradi utafanya vizuri kwani unalenga kusaidia makundi ya vijana, wanawake, pamoja na watu wenye ulemavu kwa kuwalea, kuwafunza namna ya kuzalisha kwa tija na kuwawezesha waweze kuinuka na kuwa na kipato kizuri kwa kumudu mahitaji yao ya kawaida na kupiga hatua ya maendeleo.


“Tukiangazia yale makundi yaliyopo pembezoni, mradi umeenda vijijini kabisa kwa kushirikiana na wawezeshaji wa ndani pamoja na halmashauri, ushirikiano umekuwa mkubwa pamoja na wadau wetu kuhakikisha tunapata watu sahihi,” Alisema Shoo.


Nae msaidizi wa mradi wa Tuinuke pamoja Lubengo Lubengo amesema mradi huo wa miaka 3 utafanyika Mkoa mzima wa Dodoma wakianzia Chemba na Kondoa.


Hata hivyo Mradi huo umewezeshwa na ubalozi wa Ireland hivyo matokeo wanayotarajia katika jamii wanazoenda kuzigusa zinakuwa mtambuka katika masuala ya kijinsia ili waweze kutoa haki sawa katika familia na jamii inayowazunguka.


Sambamba na hayo Lubengo amesema, “Mradi huu tumelenga kabisa kwenda kuwajengea ufahamu jamii ambazo tutakuwa tunafanya nao kazi ili ziweze kuzisaidia jamii zengine kwa kutoa elimu juu ya suala la usawa.”


Tuinuke Pamoja ni mradi wa miaka mitatu ulioanza kutekelezwa kuanzia Julai 2024 na kutarajiwa kutamatika Juni 2027 ambao pamoja na mambo mengine unalenga kuwajengea uwezo na kuviwezesha kifedha vikundi vya kijamii kuendeleza harakati zao za kuleta usawa wa kijinsia na uwezeshaji wanawake kiuchumi nchini Tanzania hususani katika Mkoa wa Dodoma.










Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA