Afisa Tathimini na Ufuatiliaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania Sylvester Mavamza kutoka Tanzania Gender Networking programme (TGNP) iliyopo Dar es salaam ameongoza semina maalumu ambayo iliendeshwa kwa njia ya mjadala yenye lengo la kuelezea usawa wa kijinsia kwa kuwafikia watu kutoka makundi mbali mbali na kuwawezesha kifedha ikiwemo watu wenye ulemavu kwa mkoa wa dodoma.
Ameyasema hayo leo January 29.2025 katika hotel ya Midland iliyopo kisasa Jijini Dodoma wakati akizungumza na Taasisi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali pamoja na waandishi na habari kwa kuweka bayana mikakati waliyoiweka ili kuwafikia watu wenye mahitaji maalumu.
Amesema baadhi ya maeneo kumekuwa na changamoto ya wazazi au walezi kuwaficha watu wenye ulemavu kwa kusema kuwa "Tutakuwa na mkakati ambao utasaidia wazazi au walezi kutoficha watu wenye ulemavu kwani na wao Wana haki za msingi kama watu wengine." Alisema Mavamza
Kwa upande wake mkurugenzi wa Foundation For Disabilities Hope (FBH) Maiko Salali ameishukuru AGAKHAN FOUNDATION kwa kushirikiana na Tanzania Gender Networking programme kwa kuanzisha mradi wa (Tuinuke pamoja) ambapo watu wenye ulemavu kushiriki moja kwa moja kwa lengo la kuwainua kiuchumi.
"Sisi tunashukuru AGAKHAN FOUNDATION kwa kushirikiana na TGNP kwakuwa wanaenda kuwasaidia na kuendelea kuwapa ushirikiano na niwaombe wale wote ambao watapata nafasi Kwenye mradi huu wa Tuinuke pamoja kwakuwa maisha ya watu yanaweza kubadilika kijamii na kiuchumi Ili kuweza na kutengeneza Taifa la pamoja lenye ushirika wa pamoja. Alisema salali
إرسال تعليق