TAKUKURU NA MISA TANZANIA WAKUBALIANA KUFANYA KAZI PAMOJA

 

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo Vya Habari Kusini Mwa Afrika ( MISA Tan) Bwana Edwin Soko Leo amemtembelea Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) Bwana Crispian Francis Chalamila na kufanya mazungumzo juu ya kufanya kazi kwa pamoja likiwemo suala la kuendelea kuwashirikisha waandishi wa habari kwenye programu ya Marafiki wa TAKUKURU.



Hatua hiyo ni mwendelezo wa uongozi mpya wa bodi ya MISA Tanzania ya kuwatembelea wadau mbalimbali kwa lengo la kujitambulisha na kupanua wigo wa kufanya kazi na wadau mbalimbali wakiwemo TAKUKURU.

Mazungumzo hayo yamefanyika kwenye ofisi za TAKUKURU Makao Makuu Dodoma

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA