Mhe. Matsawily amesema kuwa pamoja na kupanda miti, jumuiya hiyo imeendelea kufanya shughuli nyingine za kijamii, ikiwa ni sehemu ya jitihada zao za kutunza mazingira.
Amesisitiza kuwa kama jumuiya ya wazazi, watahakikisha miti hiyo inalindwa na inapata uangalizi wa kutosha ili isiharibike, kwani wanatambua umuhimu wa mazingira kwa maendeleo ya jamii.
Katika hatua nyingine, Mhe. Yassir ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake kubwa za kuleta maendeleo katika Jimbo la Bukoba Vijijini, hasa katika sekta za Afya, Elimu, Maji, miundombinu ya barabara, na miradi mingine ya maendeleo inayotekelezwa katika Mkoa wa Kagera.
Aidha, ameongeza kuwa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bukoba inajiandaa kutoa sapoti ya kutosha kwa Rais Samia na Makamu wake, Dkt. Emanuel Nchimbi, katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mapema mwaka huu.
Amesema kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia, hawatakuwa na haja ya kutumia nguvu nyingi katika uchaguzi, kwani matokeo ya uongozi wake yanadhihirika wazi kwa wananchi.
Post a Comment