BUKOBA WAPAMBANIA MAZINGIRA , ZAIDI YA MITI 280 YA MBAO YAPANDWA MAADHIMISHO MIAKA 48 YA CCM

 

Na Lydia Lugakila - Bukoba

Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera imepanda miti zaidi ya 280 ya mbao katika juhudi za kulinda mazingira. 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Halmashauri ya Bukoba, Mhe. Yassir Matsawily, ameeleza kuwa miti hiyo imepandwa katika maeneo mbalimbali ya Halmashauri hiyo kama sehemu ya kuadhimisha miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mhe. Matsawily amesema kuwa pamoja na kupanda miti, jumuiya hiyo imeendelea kufanya shughuli nyingine za kijamii, ikiwa ni sehemu ya jitihada zao za kutunza mazingira. 

Amesisitiza kuwa kama jumuiya ya wazazi, watahakikisha miti hiyo inalindwa na inapata uangalizi wa kutosha ili isiharibike, kwani wanatambua umuhimu wa mazingira kwa maendeleo ya jamii.

Katika hatua nyingine, Mhe. Yassir ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zake kubwa za kuleta maendeleo katika Jimbo la Bukoba Vijijini, hasa katika sekta za Afya, Elimu, Maji, miundombinu ya barabara, na miradi mingine ya maendeleo inayotekelezwa katika Mkoa wa Kagera.

Aidha, ameongeza kuwa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bukoba inajiandaa kutoa sapoti ya kutosha kwa Rais Samia na Makamu wake, Dkt. Emanuel Nchimbi, katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mapema mwaka huu. 

Amesema kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia, hawatakuwa na haja ya kutumia nguvu nyingi katika uchaguzi, kwani matokeo ya uongozi wake yanadhihirika wazi kwa wananchi.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA