SERIKALI KULETA GARI LA ZIADA LA ZIMAMOTO NGARA, GARI NYINGINE KUKABITHIWA MWEZI JULAI MWAKA HUU


Na, Mwandishi wetu Fichuzi news Blog - Dodoma.

Serikali imebainisha kuwa kati ya magari 150 ya Zimamoto yaliyoagizwa kwaajili ya Wilaya zote nchini Wilaya ya Ngara itakuwa miongoni mwa Wilaya zitakazopata ikiwa ni pamoja na kuongezewa watumishi/askari wa zimamoto.

Ikumbukwe kuwa wananchi wa Ngara hususani katika Mradi wa Rusumo wanatarajia kukabidhiwa gari moja la Zima moto aina ya Mercedes Benz Acros 2036 (4x2) lenye ujazo wa lita 5000 za maji na lita 500 za foam ifikapo Julai, 2025.

Majibu haya ya Serikali yametolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Daniel Sillo kufuatia swali la Msingi la Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Ndaisaba George Ruhoro alipotaka kujua mkakati wa Serikali kupeleka Gari la Zimamoto Wilayani Ngara hususani katika Mradi wa Rusumo leo Februari 14, 2025 Bungeni Jijini Dodoma.



Naibu Waziri Sillo amesema “Mradi wa Umeme wa Rusumo ulianzishwa kwa ushirikiano wa nchi tatu (3) ambazo ni Tanzania, Rwanda na Burundi, na unatekelezwa kupitia mikopo iliyotolewa na Benki ya Dunia (World Bank) na Benki ya Maendeleo Afrika (African Development Bank) ambapo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeshiriki katika hatua zote ili kuhakikisha mradi huo unakuwa salama. Katika mradi huo, limenunuliwa gari moja la kuzima moto aina ya Mercedes Benz Acros 2036 (4x2) lenye ujazo wa lita 5000 za maji na lita 500 za foam.” Amesema Naibu Waziri Sillo

Sanjari na hayo Mbunge Ndaisaba hakuchelea kutoa ombi la msisitizo kwa serikali juu ya Uhaba wa Watumishi wa zimamoto ikiwa ni pamoja na Ombi la gari la ziada “Kwakuwa gari hili limekuja mahususi kwa mradi wa Rusumo na kwakuwa mahitaji mengine ya magari ya zimamoto ni makubwa kwa kuzingatia Wilaya ni kubwa ni upi mkakati wa serikali wa kuhakikisha inatuletea gari nyingine ya ziada kwaajili ya wananchi wa jimbo la Ngara, pili Watumishi wa zimamoto ni wachache na ujio wa hii mitambo inauhitaji wao kwa kiwango kikubwa ni upi mkakati wa serikali wa kuongeza idiadi ya askari wa zimamoto pindi wananchi wa Ngara wakipata majanga ili watumike?” Aliuliza Mbunge Ndaisaba. 


Katika hatua nyingine Serikali imeonyesha nia dhabiti ya kutatua changamoto hiyo inayowakabili wananchi Wilayani Ngara ambapo Naibu Waziri amesema “Serikali imeagiza magari 150 kwaajili ya zimamoto za Wilaya zote hapa nchini hivyo Mheshimiwa Mbunge Wilaya ya Ngara itapata gari nyingine kwaajili ya zimamoto na uokoaji na katika suala la uhaba wa watrumishi wa zima moto nikiri ni kweli kuna uhaba katika baadhi ya ofisi hivyo Jeshi la Uokoaji na Zimamoto limetangaza nafasi za kazi hivi sasa au kufanya utaratibu wa watumishi wengine waende kwenye hiyo Wilaya” Alisema Mhe. Sillo




Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA