Na Mwandishi wetu - Kagera
Waziri wa Afya, Jenista Mhagama ametoa kauli hiyo leo Machi 13, 2025 wakati akihitimisha shughuli zote zilizohusu mlipuko wa ugonjwa huo ulioikumba Kata ya Ruziba, Wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera Januari 16 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu wawili.
Wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi wamefanya hafla ya kujipongeza baada ya kutumia siku 54 kuhakikisha hakuna mgonjwa mpya wala vifo kwa kutoa elimu juu ya ugonjwa wa mlipuko na kuhakikisha wahisiwa wote wanaweka karantini ili kuepusha madhara.
"Nachukua nafasi hii kuutangazia umma wa Watanzania wote na wageni kutoka nje ya nchi kuwa Tanzania ni salama na hakuna tena ugonjwa wa Marburg kwa sasa wananchi wawe huru kufanya shughuli zao bila wasiwasi nawasihi wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kwa kunawa mikono kwa kutumia maji safi na sabuni na vitakasa mikono ili kuendelea kuwa na afya njema na kujiepusha na magonjwa ya mlipuko,” amesema Mhagama.
Amesema kuwa hii ni mara ya pili mkoani Kagera kupata madhara ya ugonjwa huu ambapo kwa mara ya kwanza mgonjwa wa Marburg alipatikana katika Kata ya Maruku Wilaya ya Bukoba mkoani Kagera mwaka 2023 hivyo uwepo wa ugonjwa huo mara mbili mfululizo kumeifanya serikali za kuchukua hatua kadhaa ili kuhakikisha inakabiliana na ugonjwa wa mlipuko.
إرسال تعليق