Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Joyce Shebe akizungumza kwenye Mkutano wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN) na wadau wa habari
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Joyce Shebe akizungumza kwenye Mkutano wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN) na wadau wa habari
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Joyce Shebe, amesisitiza umuhimu wa amani na usawa kwa wanawake wakati wa uchaguzi huku akihamasisha wanawake kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi za uongozi wakati wa uchaguzi Mkuu mwaka 2025.
Akizungumza leo Machi 14,2015 jijini Dodoma katika Mkutano wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-TAN) na wadau wa habari, Shebe amesema kuwa usalama wa jamii ni sawa na usalama wa mwanahabari, na kuongeza kuwa ni muhimu kuwepo na mazingira ya amani na usawa katika upatikanaji wa habari.
Mwenyekiti huyo amesema uwepo wa amani na utulivu utahamasisha Wanawake wengi kushiriki katika hatua zote za uchaguzi.
"TAMWA tunaendelea kuhamasisha upatikanaji wa taarifa sahihi na kwa wakati kwenye mchakato wa uchaguzi ili makundi yote katika jamii yaweze kuelimika na hatimaye wafanye maamuzi sahihi", ameeleza.
Shebe ameeleza kuwa wanawake wagombea mara nyingi wanarudi nyuma wakishuhudia udhaliliahaji mitandaoni na kwenye majukwaa ya kisiasa, hivyo tunatoka wito kwa jamii kuitumia vizuri majukwaa hayo kwa kuheshimu utu wa mtu.
"TAMWA inaendelea kusisitiza kuwa mgombea mwanamke ni sawa na mgombea wa mwanaume, hivyo Wanawake wapimwe kwa uwezo wao na si vinginevyo", amesema
Shebe.
إرسال تعليق