Na Lydia Lugakila -Kyerwa
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera, Faris Buruhani, amewataka wananchi katika Kata ya Kibingo, Wilayani Kyerwa, Mkoani Kagera, kuacha tabia ya kuwachagua viongozi wa vyama vingine, na badala yake wachague Chama cha Mapinduzi (CCM), ambacho kimeleta mageuzi makubwa.
Akizungumza kuhusu mageuzi hayo, Faris ametaja hasa katika zao kubwa la Mkoa wa Kagera, ambalo ni zao la kahawa. Amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameliboresha kwa kulipa heshima kubwa na kulipandisha bei.
Akizungumza na baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM katika Ofisi ya Kijiji cha Rwenkende, Kata ya Kibingo, Wilayani Kyerwa, Mkoani Kagera, wakati wa ziara ya siku 16 ndani ya mkoa huo, ambapo lengo lilikuwa ni kutafuta kura mpya kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Faris amesema wananchi na wanachama wa CCM wanatakiwa kuacha mazoea ya kuwachagua viongozi wa vyama vingine, na badala yake wachague viongozi wanaotokana na CCM.
Faris ameongeza kuwa Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya mageuzi ndani na nje ya Mkoa wa Kagera.
Ametolea mfano bei ya zao la kahawa, ambapo bei imepandishwa kutoka shilingi 1,200 hadi shilingi 5,000, na kusema kuwa wananchi wa Kata ya Kibingo wanatakiwa kumlipa Rais Samia kwa kumpigia kura za kutosha wakati wa uchaguzi.
Aidha, ametoa wito kwa wanachama wa CCM katika Kata ya Kibingo kutokuweka usaliti wa aina yoyote wakati uchaguzi mkuu unapokaribia, bali wawe na mapenzi mema kwa wagombea wa CCM, kwani CCM ndicho chama kitakachowaletea maendeleo.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi na wanachama wa CCM wamesema kuwa wakati wa uchaguzi mkuu, watajitokeza kwa wingi kumpigia kura Rais Samia, kwa sababu amewapambania hadi kupandisha bei ya zao la kahawa na kuleta miradi mikubwa ya maendeleo.
إرسال تعليق