CCM YAFANYA MABADILIKO YA RATIBA YA UCHUKUAJI9 NA UREJESHAJI WA FOMU ZA KUOMBA KUWANIA UDIWANI NA UBUNGE


Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza mabadiliko ya ratiba ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuomba kuwania udiwani, uwakilishi na ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.


Taarifa kwa umma iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Jumatano, Aprili 16, 2025 na Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi imeeleza uamuzi wa kubadili ratiba hiyo umetokana na mashauriano na wanachama wake na kutafakari kwa kina hivyo, kimeamua kusogeza mbele ratiba hiyo.

Dk Nchimbi amesema shughuli hiyo sasa itaanza Juni 28 hadi Julai 2, 2025 saa 10 jioni.

Fomu hizo zitakuwa kwa makatibu wa jumuiya za chama hicho zikiwamo UWT, UVCCM na Wazazi ngazi za mikoa kwa nafasi ya viti maalum za ubunge na ujumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Ubunge na Ujumbe wa Baraza la Uwakilishi, fomu hizo zitatolewa na Makatibu wa CCM wa wilaya.

Ratiba iliyotolewa Aprili 10, 2025 na Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla ilieleza uchukuaji na urejeshaji wa fomu hizo ungeanza Mei Mosi hadi 15, 2025.

Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 تعليقات

إرسال تعليق

Post a Comment (0)

أحدث أقدم

TUTUMIE UJUMBE HAPA