SERIKALI KUANZA KUNUNUA MAHINDI NGARA KUANZIA MWEZI MEI, 2025


Na, Mwandishi wetu - Fichuzi news blog.

Serikali imeweka bayana kuanza rasmi zoezi la ununuzi wa mahindi ikiwemo katika Jimbo la Ngara kuanzia Mwezi Mei, 2025 huku wananchi wakisisitizwa  kuzingatia usafi wa mahindi na kukausha mahindi yao hadi kufikia kiwango cha unyevu wa 13.5% ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza endapo mahindi yao hayatakidhi ubora unaohitajika.


Majibu hayo ya Serikali yametolewa na Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. David Silinde kufuatia swali la Mbunge wa Jimbo la Ngara Mheshimiwa Ndaisaba George Ruhoro alilouliza leo Aprili 14, 2025 bungeni Jijini Dodoma alilouliza kuwa "Je, ni lini Serikali itaanza kununua mahindi ya wananchi wa Jimbo la Ngara kupitia NFRA."


"Zoezi la ununuzi wa mahindi ikiwemo Jimbo la Ngara linatarajia kuanza mwezi Mei, 2025. Wakulima wanasisitizwa kuzingatia usafi wa mahindi na kukausha mahindi yao hadi kufikia kiwango cha unyevu wa 13.5% ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza endapo mahindi yao hayatakidhi ubora unaohitajika." Amesema Naibu Waziri Silinde
Je?, UNA HABARI,PICHA, TANGAZO AU TAARIFA AMBAYO UNGEPENDA TUICHAPISHE KATIKA MTANDAO HUU? WASILIANA NASI, Email : fichuziblog@gmail.com , Simu +255 752 925 603

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post

TUTUMIE UJUMBE HAPA