Na, Mwandishi wetu - Fichuzi news blog.
Serikali imeweka bayana kuanza rasmi zoezi la ununuzi wa mahindi ikiwemo katika Jimbo la Ngara kuanzia Mwezi Mei, 2025 huku wananchi wakisisitizwa kuzingatia usafi wa mahindi na kukausha mahindi yao hadi kufikia kiwango cha unyevu wa 13.5% ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza endapo mahindi yao hayatakidhi ubora unaohitajika.
Majibu hayo ya Serikali yametolewa na Naibu Waziri Wizara ya Kilimo Mhe. David Silinde kufuatia swali la Mbunge wa Jimbo la Ngara Mheshimiwa Ndaisaba George Ruhoro alilouliza leo Aprili 14, 2025 bungeni Jijini Dodoma alilouliza kuwa "Je, ni lini Serikali itaanza kununua mahindi ya wananchi wa Jimbo la Ngara kupitia NFRA."
"Zoezi la ununuzi wa mahindi ikiwemo Jimbo la Ngara linatarajia kuanza mwezi Mei, 2025. Wakulima wanasisitizwa kuzingatia usafi wa mahindi na kukausha mahindi yao hadi kufikia kiwango cha unyevu wa 13.5% ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza endapo mahindi yao hayatakidhi ubora unaohitajika." Amesema Naibu Waziri Silinde
إرسال تعليق